Hedhi Kila mwezi kuna mabadiliko ya homoni ambayo huuandaa mfuko wa uzazi ‘uterus’ kutengeneza ukuta mpya ‘endometrium’ kwa ajili ya kujiw...
Hedhi
Kila mwezi kuna mabadiliko ya homoni ambayo huuandaa mfuko wa uzazi ‘uterus’ kutengeneza ukuta mpya ‘endometrium’ kwa ajili ya kujiweka tayari kwa mapokezi ya mimba inayoweza kutungwa.
Kama yai litaachiliwa na kutorutubishwa na mbegu za mwanamme, basi ukuta wa mfuko wa uzazi humeguka na kutoka nje ukiwa pamoja na damu kupitia ukeni.
Kitendo hiki cha mzunguko hadi kutoka kwa damu ndicho huitwa hedhi (menstruation) au mzunguko wa hedhi (menstrual cycle).
mzunguko wa damu umegawanyika katika maeneo makuu mawili.
1.MZUNGUKO WA DAMU UNAOPEVUSHA MAYAI (OVULATORY CYCLE).
2.MZUNGUKO WA DAMU USIOPEVUSHA MAYAI (ANOVULATORY CYCLE).
Napenda tufahamu kwa kina mizunguko hii.
MZUNGUKO WA HEDHI UNAOPEVUSHA MAYAI (OVULATORY CYCLE).
katika mzunguko huu mwanamke hutokwa na ute ute wa Uzazi ambao unavutika na katika mzunguko huu mtu anaweza kupata ujauzito
MZUNGUKO WA HEDHI USIOPEVUSHA MAYAI (ANOVULATORY CYCLE).
katika mzunguko huu mwanamke hatoki ute ute wa Uzazi hivyo hawezi kupata ujauzito.
~ pamoja na mizunguko hii miwili kutofautiana mwanamke hupata hedhi kama kawaida hata hivyo mwanamke ambaye mzunguko wake wa Hedhi hapati ute ute wa Uzazi hawezi kupata ujauzito kutokana na mabadiliko ya mfumo wa homoni
pia napenda mfaham kuwa ute ute wa Uzazi umegawanyika katika Makundi makuu matatu ambayo ni
UTE MWEPESI
UTE UNAOVUTIKA
UTE MZITO
Mara nyingi wanawake wasiopevusha mayai hawawezi kupata ujauzito hivyo huwa hawapati ute wa Uzazi na pia wengine hupata ute mzito daima kama uchafu unaotoka ukeni Lakini wenyewe hauna harufu wala muwasho
Mzunguko wa kawaida ni upi ?
Mzunguko wa hedhi huanzia siku ya kwanza ya kutoka kwa damu hadi siku ya kwanza tena ya kutoka damu ya mzunguko unaofuata.
Japokuwa mzunguko wa hedhi wa kawaida ni siku 28, ni jambo la kawaida kuwa na mzunguko wenye siku pungufu au zaidi ya hizo.
Mzunguko huu huweza kutofautiana kati ya wanawake lakini pia kati ya mzunguko mmoja na mwingine.
Mzunguko wa kawaida huwa na siku 21 hadi siku 35 kwa wanawake wakubwa na siku 21 hadi 45 kwa wasichana wadogo walioanza hedhi.
Kwa miaka michache ya awali baada ya msichana kupata hedhi yake ya kwanza (kuvunja ungo), kupata mizunguko mirefu huwa ni jambo la kawaida.
Mizunguko huanza kupungua urefu (idadi ya siku) na kuanza kuwa ya kawaida kadri umri unavyosonga na mara nyingi mzunguko huwa kati ya siku 21 hadi 35.
Msichana huanza kupata hedhi (period) wakati gani ?
Kwa kawaida, msichana huanza kupata hedhi ya kwanza (menarche) afikapo umri wa miaka 11-14. Hata hivyo, hedhi huweza pia kutokea binti angali na miaka 8 na hali hii huwa ni kawaida pia.
Umri wa wastani ni miaka 12 lakini hii haimaanishi kwamba wasichana wote hupata hedhi ya kwanza katika umri sawa.
Mara nyingi hedhi ya kwanza huanza miaka miwili baada matiti ya binti kuanza kutokeza. Iwapo binti hajapata hedhi ya kwanza angali na miaka 15 au ni miaka 2 hadi 3 baada ya kuanza kuota matiti, anapaswa amuone daktari.
Ukomo wa hedhi ni wakati gani ?
Mwanamke huanza kupata ukomo wa hedhi (menapause) anapofika umri kati ya miaka 45-55. Wanawake wengine hupata ukomo wa hedhi angali na umri mdogo zaidi kwa sababu mbalimbali ikiwemo kufanyiwa upasuaji au baadhi ya matibabu, kuugua au sababu nyingine.
Katika hali ya kawaida, mwanamke huanza kupata hedhi chache anapofika umri wa miaka 40 ambapo huanza kupata mizunguko mirefu na inayobadilika mara kwa mara.
Mizunguko huanza kuwa mirefu na baadaye kukoma kabisa.
Hedhi ya kawaida ni ipi ?
Wakati wa hedhi, mwanamke hutokwa na mchanganyiko wa damu pamoja na ukuta wa mfuko wa uzazi uliomeguka kupitia sehemu ya uke. Kiasi cha damu inayotoka (menstual flow) huweza kutofautiana kati ya mizunguko.
Kwa wastani mwanamke hutokwa na damu ya hedhi kiasi cha ujazo wa mililita 35 (sawa na vijiko viwili na nusu vya chai).
Hata hivyo, kutokwa na damu inayofikia mililita 10 hadi 80 (kijiko 1 hadi vijiko 6) bado huchukuliwa kama hali ya kawaida.
Wanawake wengi hupata hedhi inayodumu kwa siku 3-5, lakini hedhi yoyote inayodumu siku 2-7 huwa ya kawaida.
Kabla ya hedhi kuanza, wanawake wengi hupatwa na dalili mbali mbali
Fuatilia masomo haya
Maisha ni afya
COMMENTS